Picha

Picha: AY na Mrisho Mpoto watoa mada kwenye semina ya kuchangamkia fursa Kigoma

Ambwene Yesaya aka AY na Mrisho Mpoto walikuwa miongoni mwa wasanii walioshiriki katika kutoa mada kwenye semina ya kuchangamkia fursa zilizopo nchini iliyofanyika mkoani Kigoma wiki iliyopita.

5
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na mfanyabiashara,Ambwene Yesaya a.k.a AY akitoa ushuhuda wake na mifano mbalimbali katika Semina ya Fursa,kuhusiana na fursa alizozipata na kuzifanyia kazi,na kumpelekea mafanikio aliyonayo mpaka sasa

Semina hizo zimedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel ili kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini zitakazoendeshwa kwenye zaidi ya mikoa 13 kwa kushirikiana na Clouds Media Group.

1
Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko

Semina hizo ambazo zinaenda sambamba na ziara ya kimuziki ya tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu litaenda zaidi ya mikoa 13, zinatarajiwa kufanyika siku moja kabla ya tamasha kila mkoa ambao Fiesta inaenda.

2
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya wakati wa uzinduzi wa semina ya Fursa,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa

Mada zitakazojadiliwa kwenye semina hizo ni pamoja na ubunifu, ujasiriamali, Uongezaji thamani kwenye bidhaa au shughuli yoyote unayofanya pamoja na kujenga ushirikiano, uwekezaji pamoja na lugha.

3
Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY

Akizungumzia semina hizo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amesema kampuni yake imekuwa msitari wa mbele katika kuwawezesha vijana, na kwa semina hizi wanaamini vijana wengi watapata nafasi ya kuzitambua na kujifunza.

‘Tanzania ina fursa nyingi sana kwa vijana, na sisi Zantel tunaamini nafasi hii itakuwa muhimu kwa vijana kujifunza na kutambua fursa zilizopo kutoka kwa wataalamu mbalimbali’ alisema Khan.

4
Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi wa mji wa kigoma,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali

Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alisema nchi ya Tanzania ina fursa nyingi lakini tatizo limekuwa ni namna ya kuzitumia fursa hizo.

‘Tumeandaa semina hizi kwa kutambua tatizo kubwa lilipo kwenye jamii yetu, umaskini na ukosefu wa ajira kwa vijana, jambo ambalo semina hizi zitaenda kutatua’ alisema Mutahaba.

6
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa semina ya Fursa

Mojawapo wa wazungumzaji kwenye semina hizo atakuwa Mrisho Mpoto, mwakilishi wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Ruge Mutahaba pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.

7

8

Kwa mwaka huu semina hizo zimeanzia mkoa wa Kigoma, katika Ukumbi wa Kibo Hall Park, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents