Burudani

Picha: Baada ya Shilole kufunga ndoa Nuh Mziwanda atupa kijembe

Hatimaye msanii wa muziki Shilole amefungua ndoa na mpenzi wake Uchebe.

Mara kadhaa Shilole alikuwa akisisitiza kufunga ndoa mwaka huu lakini watu walikuwa wakichukulia poa kwa sababu si mara ya kwanza kutoa kauli kama hiyo lakini hapo jana December 6 akafanya kweli.

Baada ya picha kusambaa mtandaoni aliyekuwa mpenzi wa Shilole, Nuh Mziwanda ameandika ujumbe katika ukurasa wa Instagram ambao unaweza kutafsiriwa kama ametupa kijembe kwenye ndoa hiyo, Nuh ameandika;

Alie LaLa na BiBi harusi’wiki Moja KabLa ya harusi’Na wala sio Bwana Harusi’Bado mnanishauri harusi 😏 (all girls are pretenders )

Alichokiandika Nuh Mziwanda ni mistari kutoka kwenye wimbo wa Mwana FA ‘Bado Nipo Nipo’ ambao ulitoka takribani miaka 10 iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents