Burudani ya Michezo Live

Picha: Baba mzazi wa Pam D azikwa Njombe

Baba yake mzazi na msanii wa Bongo Flava, Pam D, Shedrack Nyato amezikwa Ijumaa hii nyumbani kwao, mkoani Njombe.

Nyato alikuwa mpiga gitaa mahiri aliyewahi kufanya kazi na msanii wa DRC, Kanda Bongo Man.

“Umuhimu wake ni zaidi ya chochote, maneno yake hayakuwa ya kunivunja moyo, milikuwa nahofia kesho, akanipa moyo wa kujiamini, milimuomba Mungu asitangulie, Yeye alikuwa akiniombea maisha marefu,” amesema Pam D.

Baba yake Pam D (anayepiga gitaa) akitumbuiza pamoja na bendi ya Kanda Bongo Man

Alhamis hii, Bongo Man alimtumia ujumbe wa WhatsApp Pam D na kumuomba asome maneno aliyoandika kabla hajazikwa.

“Hey Festo jamaa yangu, tulisafiri wote Marekani, Canada, Zimbabwe, Visiwa vya Komoro, Mayotte, Reunion Island, Malawi na Australia. Hukuwa tu mwanamuziki bora niliyekutana naye katika maisha yangu lakini mmoja wa wanamuziki niliowachagua kutumbuiza pembeni yangu. Mungu akubariki na lala salama. Ujumbe toka kwa Bongo Man,” aliandika kwenye ujumbe huo.

“Unaweza kusoma ujumbe huu kwa Festo wakati ukiongea kabla ya kumzika. Asante sana,” alisisitiza.

Naye Pam D aliscreenshot ujumbe huo na kuweka picha Instagram akiandika, “Rip daddy……..natamani ungekuwa hai uskie haya maneno mwenyewe bila kupatiwa hizi salam ukiwa umelala milele, #rip my papaa #mostlytalented #thanxkanda.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW