Burudani

Picha: Baba Wa Msanii Ditto Aagwa Jana Alasiri

Msanii Ditto Lameck Mkwama jana mchana ameongoza ndugu,jamaa na marafiki katika misa ya kumuombea marehemu baba yake aliyefariki usiku wa kuamkia jana. Misa hiyo ya kumuaga baba mzazi wa msanii huyo ilifanyika katika kanisa la Muhimbili Jijini Dar-Es-Salaam jana mchana majira ya saa tisa alasiri.

Pamoja naye kumuaga baba Yake Ditto walikuwa wana THT wakiongozwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo ya Burudani Bwana Ruge Mutahaba, wasanii Nash, Amini na wafanyakazi wa taasisi hiyo ambao wamekuwa na Ditto kwa takriban miaka miwili na nusu tangu msanii huyo kuhamia katika kundi hilo akitokea kundi la La Familia Ilala linaloongozwa na Chidi Benz.

Baba wa Msanii Ditto Marehemu Lambert Mkwama amefariki akiwa na umri wa miaka 53, na anatarajiwa kuzikwa leo mkoani Morogoro ambako ndipo maskani yake yalipokuwa.

Bongo5 inaungana na familia ya ndugu, jamaa na marafiki wa Ditto katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Lambert Mkwama . Amin

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents