Bongo Movie

Christian Bella atuzwa zaidi ya sh 15 milioni katika show ya ‘The Black Tie’ ya Wema Sepetu

Mkali wa masauti Christian Bella ameendelea kuonyesha ukongwe wake katika show ya ‘The Black Tie’ iliyofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa King Solomon jiji Dar es salaam.
Bella
Bella akijazwa madola

Muimbaji huyo mwenye asili Kongo, alionyesha uwezo wake mkubwa wa kuimba hali ambayo iliwafanya mashabiki ambao walijitokeza katika show hiyo kutoa pesa zao mfukoni na kumtuza msanii huyo.
Bella akikusanya mshiko kwanza
Akikusanya mapato ya kutuzwa

Akiwa mwenye furaha jukwaani, Bella alisema pesa ambayo ametuzwa jukwaani kwa usiku huo zinatosha kumpeleka Afrika Kusini na kushoot video mpya.

“Nashukuru mungu nimepata hela ya video, asanteni sana mashabiki wangu,” alisema Bella huyu akipiga magoti kumshukuru mungu.

Kwa upande wa muandaaji wa show hiyo, Wema Sepetu kupitia instagram yake, amempongeza msanii huyo huku akitaja kiwacho cha pesa alichotuzwa.

“7000$ alitunzwa jana Mzee wa Masauti… Jamani tusubirie Pictures eeh…. They are coming soo,” aliandika Wema.

Ukiachana na dola hizo, mashabiki wake wengine pamoja na wasanii wa filamu wakiongozwa na Steve Nyerere, JB pamoja na Irene Uwoya alishindana kumtuza msanii huyo.

Kiingilio katika show hiyo, kilikuwa ni tsh 50,000 kwa viti vya kawaida huku VIP iliwa tsh 100,000 na milioni 1 kwa meza nzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents