Burudani

Picha: Cookie wa Empire apata shavu jingine

Wengi wanamfahamu kama Cookie hasa kupitia tamthilia ya Empire, ila jina lake halisi ni Taraji P. Henson ambaye amekuwa akipata mashavu kila kukicha na jingine limemdondokea kipindi hiki.

Mrembo huyu anayetikisa Hollywood kwa sasa, anatarajiwa kuonekana amekava  jarida la Marie Claire,  ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu na kupitia jarida hilo tutegemee kufahamu balimbali kuhusiana na vitu alivyotamani kuviacha, mahusiano pamoja na sababu zinazomfanya aonekanae bado kijana.

Cookie mwenye miaka 47 pia ataeleza juu ya jitihada zake anazofanya katika kuhakikisha anasaidia wanawake wengine katika tasnia hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents