Burudani ya Michezo Live

Picha: Dar Shapers waandaa mahafali ya waathirika wa madawa ya kulevya

Taasisi ya Global Shapers Dar Es Salaam Hub Leo imeandaa mahafali kwa ajili ya waathirika wa madawa ya kulevya,ikiwa ni hitimisho ya mafunzo ya biashara walizokua wakipewa na vijana wa taasisi hiyo. Global Shapers, wakishirikiana na kituo cha South Beach Sober House iliyopo Kimbiji, Kigamboni, waliandaa mafunzo yaliyopitishwa na shirika la kazi duniani, kufundisha Ujasiriamali pamoja na mafunzo ya vigezo vya kuajiriwa.

Katika mahafali hayo, Dr. Lwidiko Edward, Akizungumza kwa niaba ya Global shapers Daresalaam, amesema kwamba, ni muhimu kuweza kutoa mafunzo hayo kwa waathirkia wa madawa ya kulevya ili kuweza kutoa mbinu mbadala za kuishi ikiwemo ujasiriamali na uwezo wa kuajiriwa.

Aliongeza kwa kusema kwamba, “Kuanzia sasa, tunategemea kusikia habari za mafanikio kimaisha na kibiashara kutoka kwa wahitimu waliotunukiwa vyeti katika mahafali hayo.

Global Shapers Dar es Salaam, wametoa rai kwa wanajamii wote kutokuwanyanyapaa waathirika wa madawa na pia kutoa wito kwa taasisi mbalimbali kuweza kushirikiana na serikali kuwasaidia vijana walioathirika kujikwamua kutoka Kwenye janga hilo

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW