Burudani

Picha: Davido ala bata na mrembo huyu wa Tanzania

Kwa wanakijiji wa Instagram, Tuerny si mgeni katika macho yao.

Ni mrembo ambaye profile yake inaonesha kuwa ni makeup artist. Anafahamika kwa kuishi maisha ya kula bata na kusafiri kila leo.

Inasemekana kuwa mrembo huyo ni moja ya warembo ambao staa wa Nigeria huwafaidi kwa muda tu. Vyanzo vilivyo karibu na mrembo huyo vinadai kuwa wamekuwa pamoja kwa takriban miaka minne na uhusiano wao ni ule wa ‘friends with benefit’ kwamba kila mmoja ana maisha yake, wakimisiana basi mrembo hula flight kukutana na Davido na kupeana raha.

Wawili hao wamekutana wiki iliyopita na picha yao wakiwa pamoja imesambaa mtandaoni.

“Kwenye instastory yake wapo kitandani Davido kavaa bukta naona pale walikuwa wanachukua video tu,” ameandika shabiki mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents