Burudani

Picha: Dola milioni 1 zapukutika kwenye sherehe ya birthday ya Mugabe

Kiasi cha dola milioni moja za Marekani, zimetumika kuandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aliyetimiza umri wa miaka 91.

APTOPIX Zimbabwe Mugabe Birthday Celebrations

Sherehe hiyo ilifanyika Jumamosi iliyopita kwenye hoteli ya kifahari (Elephant Hill) iliyopo karibu na maporomoko ya Victoria katika mto Zambezi.

Grace Mugabe looks on next to her husband Robert Mugabe during his 91st birthday celebration in Victoria Falls

Rais Mugabe ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani huku akitarajia kuwania nafasi nyingine hadi mwaka 2018. Wafuasi wake katika chama tawala cha ZANU-PF wameahidi kuendeleea kumuunga mkono kiongozi wao aliyetawala tokea walivyopata uhuru.

Zimbabwe Mugabe Birthday Celebrations

Wamesema wataendelea kumpa nafasi kwa kipindi kingine bila kujali afya yake ambayo imeendelea kuzorota kila siku bila kusahau kudondoka kwake siku chache zilizopita huku akiwarushia lawama walinzi wake kwa kutokuwa makini na kazi yao.

Zimbabwe Mugabe Birthday Celebrations

Kwenye sherehe hiyo, watu walikula na kunywa vya kutosha katika birthday hiyo kubwa na keki nyingi za kutosha zilikatwa huku mzee huyo akitumia siku huyo kuwarushia lawama na shutuma nyingi Wamarekani.

Zimbabwe Mugabe Birthday Celebrations

Vile vile Kiongozi huyo aliingia akiwa kwenye gari la kifahari la zamani lililotengenezwa mwaka 1955, Ford Modeo.

Zimbabwe Mugabe Birthday Celebrations

Chama cha upinzani nchini humo hakikukubaliana na sherehe hiyo iliyotumia fedha nyingi za umma huku watu wengi wakiwa kwenye umaskini na huduma mbaya kwenye hospitalini.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents