Burudani
I woke up in a new Bugatti: Drake aunesha ‘mdoli wake mpya’ Bugatti Veyron (Picha)
Started from the bottom to Bugatti! inaweza kuwa remix ya vitendo kwa rapper kutoka Canada Drake ambaye ana mchuma mpya na wa gharama aina ya Buggatti alioanza kuonekana nayo ahamisi iliyopita huko kwao Canada.
Siku ya alhamisi (June 6) iliyopita Drizzy aliweka picha ya gari yake mpya na ya gharama Bugatti Veyron nyeusi ya kung’aa ambayo inakadiriwa kuwa ya kiasi cha $ 2 Million na kuandika caption “It’s levels to thi…never mind. #SangNoir #ShouldHaveBeenASoccerPlayer #EuroLifestyle #CreamsicleGuts”