Habari

Picha: GLF yakabidhi zawadi nono kwa wanafunzi bora Zanzibar

By  | 

Ijumaa hii taasisi ya Green Light Foundation, iliyopo kisiwani Zanzibar kupitia kwa Mwenyekiti wake Salim Omari Musa, wamekabidhi computer tatu kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao ya sayansi kitaifa huku viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria sherehe hizo akiwemo Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mahmoud ambaye alikuwa mgeni rasmi.


Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mahmoud akimkabidhi zawadi ya laptop mmoja ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa

Mwenyekiti huyo amekabidhi computer aina ya laptop hizo leo na kuwataka wanafunzi hao ambao ni Rwahda Ramadan, Mickdady Mohamed na Ally Nassor.


Mwenyekiti wa Green Light Foundation aliyevaa suti ya rangi ya blue akiwa na viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwemo Waziri wa Fedha [wakwanza kulia]

Naye mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe. Ayoub aliwataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa hiyo waliyoipata kutoka katika taasisi hiyo pamoja na serikali pamoja na kuipongeza taasisi hiyo kwa kujitolea kusaidia kuwasomesha wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kupata elimu kwa kukosa fedha za malipo.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments