Habari

Picha: GLF yatoa msaada wa chakula katika shule zilizopo Zanzibar

Taasisi ya Green Light Fondation (GLF) imetoa msaada wa chakula katika shule ya Sekondari Kiembe Samaki ya iliyopo kisiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa GLF , Salim Mussa Omar akikabidhi misaada kwa wanafunzi

Akikabishi msaada huo Mwenyekiti wa taasisi hiyo Salim Mussa Omar ameziaka jamii pamoja na wadau wa elimu nchini kujenge mazoea ya kusaidia katika Shule ilikuwafanya wanafunzi wapate hamasa ya kupenda na kuudhuria shuleni na kuleta ushindani katika masomo.

GLF, imekuwa moja ya taasisi kubwa kisiwani hapo kutoa misaada mbalimbali katika nyanja mbalimbali hususani katika elimu, miongoni mwa shule zilizopata msaada wa chakula kutoka taasisi hiyo ni Lumumba, Gando, Shaviani na Madungu.

Mwenyekiti wa GLF , Salim Mussa Omar akisisitiza jambo kwa wanafunzi

“Huwezi kujenga jamii imara bila kuweza kuweka misingi ya elimu vizuri hatuwezi kuwa na taifa lililoendelea bila kuwa vijana waliondelea kielimu” Alisema Bw Salim Mussa.

Kwa upande wa wanafunzi wa shule hiyo wameshukuru kitendo hicho ,nakusema kuwa kufanya hivyo imeonesha ni jinsi gani jamii ianavyowajali, na kuomba wadau waendelee kuwapa misaada ili waweze kufanya vizuri mitihani yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents