Habari

Picha: Huyu ndiye aliyeichukua nafasi ya Mr. T Touch ndani ya studio ya Free Nation ya Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amemtambulisha producer mpya wa studio yake Free Nation Record baada ya kuachana na Mr T Touch.

Producer huyo akiwa ndani ya Free Nation Record

Rapper huyo ameonekana akiwa studio na producer huyo aitwae Osam wakirekodi wimbo mpya.

Producer huyo kupitia taarifa aliyoitoa kupitia Instagram, amedai amesainiwa studio hiyo ya Free Nation Record kama producer wa studio.

Nay wa Mitego na Mr T Touch wanadaiwa kuachana baada ya kushindwana kibiashara ambapo kwa sasa producer huyo amefungua studio mpya iliyopo Sinza Jijini Dar es salaam. Angalia picha za studio hiyo.

Nay wa Mitego akiandaa kazi mpya ndani ya studio hiyo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents