Burudani

Picha: I Miss You ya Lady Jaydee kuanza kuonekana Ijumaa hii

Ni muda mrefu mashabiki wametamani kumsikia tena Lady Jaydee baada ya ukimya wake wa takribani miezi mitano.

Hatimaye malkia huyo wa Bongo Flava, Jumanne hii ameachia wimbo wake mpya ‘I Miss You’ ambayo imetayarishwa na Man Walter. Lakini bado kiu ya mashabiki wanatamani kuiona video ya wimbo huo.

Akiongea na Bongo5, mmoja ya watu wa karibu wa msanii huyo amesema, video ya wimbo huo itatoka rasmi siku ya Ijumaa hii na imeongozwa na Justin Campos nchini Afrika Kusini.

Video ya mwisho ya Jide ilikuwa ni ‘Rosella’ aliyofanya na kundi la H_art The Band kutoka nchini Kenya ambapo pia wimbo huo unapatikana katika albamu yake mpya, Woman. Hizi ni baadhi ya picha zinazoweza kuonekana katika wimbo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents