Habari

Picha: Irom Sharmila kusitisha mgomo wake wa kula chakula baada ya miaka 16

Mwanaharakati nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake wa kukataa chakula dhidi ya sheria tata baada ya miaka 16.
FSPA-indialivetoday

Mwanaharakati huyo anatarajia kuanza kula hii leo baada ya mahakama katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo la Manipur kumuachilia huru leo.

Amekua katika mahabusu ya mahakama na kulazimishwa kula kupitia mrija kupitia pua lake kuepuka sheria inayoadhibu uhalifu wa kutaka kujiua.

Lakini mwezi uliopita aliiambia mahakama kwamba anataka kukatiza mgomo wake na kuanza kampeni yake kama mgomea huru katika uchaguzi ujao wa wabunge .

Bi Sharmila amekua akipinga sheria inayopatia jeshi mamlaka maalum (AFSPA), ambayo inawapatia wanajeshi mamlaka yote ya kuwakamata watu bila vibali na hata kupiga risasi kwa lengo la kuua katika majimbo kadhaa nchini India , likiwemo jimbo la Manipur na la Kashmir.

Mpiga picha Ian Thomas Jansen-Lonnquist alifuatilia kwa karibu safari yake katika miaka michache iliyopita.

_90710131_8c26fdd8-9b7c-45d4-881c-67e445d3c522
Ndani ya chumba cha Irom Sharmila Chanu aliwekewa mchanganyiko wa dawa uliochanganywa na maziwa ya unga ya watoto ambao alilishwa kwa mrija kwa nguvu. Mchanganyiko huo uliighalimu serikali wastani wa dola $500 kwa wiki

_90710133_e46f4479-a2dd-4e78-8641-0e8c61cb499c
Bi Chanu akiwasili kutoka eneo alikoshikiliwa la hospitali ya taasisi ya sayansi ya tiba (JNIMS)chini ya ulinzi mkali wa polisi akielekea kwenye kesi yake iliyosikilizwa mara mbili kwa wiki katika mahakama ya juu ya Imphal, jimbo la Manipur kaskazini mashariki mwa India , kuelezea msimamo wake wa miaka 14 wakati huo wa kugoma chakula kupinga sheria inayopatia mamlaka ya ziada jeshi.


Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents