Picha
Picha: Jamie Foxx kuigiza adui (villain) kwenye The Amazing Spider-Man 2
Kama wewe ni shabiki wa Jamie Foxx, tegemea kumuona akicheza adui, tena wa kutisha kwenye The Amazing Spider-Man 2.
Kwenye filamu hiyo ya action inayoongozwa na Mark Webb, Jamie ataigiza kama Maxwell Dillion akiwa na waigizaji wengine Andrew Garfield na Emma Stone.
Jamie ataigiza kama fundi umeme ambaye atapigwa na radi na kupata uwezo wa kucontrol umeme. Matokeo ya kupigwa kwake shoti yanasababisha kumfanya awe mtu mbaya, Electro. The Amazing Spider-Man 2 itaingia sokoni nchini Marekani May 2, 2014.