Picha: Japan yaacha ujumbe wa shukrani ‘dressing room’ na kufanya usafi uwanja mzima

Timu ya taifa ya Japan imeonyesha mfano wa kuigwa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi baada ya kuacha ujumbe wa shukrani kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kufanya usafi uwanja mzima ambao wamechezea mechi yao hapo jana dhidi ya Ubelgiji.  

Licha ya kupokea kipigo cha jumla ya mabao 3 – 2 dhidi ya Ubelgiji na kuyaaga mashindano Japan imeonyesha mfano huo wa kuigwa na mataifa yaliyoshiriki baada ya kuhakikisha wamesafisha chumba chao cha kubadilishia nguo huku maelfu ya mashabiki wakifanya usafi kwenye uwanja waliyochezea hapo jana jambo ambalo ni nadra kufanywa na timu shiriki.

Wachezaji wengi wa Japan walionekana wakibubujikwa na machozi baada ya kutolewa kwenye mashindano hayo kwa bao la mwisho la Nacer Chadli na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 3 – 2 dhidi ya Ubelgiji.

Taarifa kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA kupitia ukurasa wake wa Twitter umeandika kuwa kikosi cha Japan kimeacha ujumbe wa shukrani kwa waandaji wa mashindano hayo Urusi.

Japan's supporters would have been forgiven for making a fast exit after losing their match

Japan scorer Genki Haraguchi covered his face with a towel when the final whistle was blown

Japan midfielder Takashi Inui (left), who also scored, needed consoling after full-time

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW