Burudani

Picha: Jay Z na Beyonce wanunua mjengo mpya walioutolea macho muda mrefu

Jay Z na Beyonce ni kama tayari wameshajitengenezea pepo yao ya duniani. Mastaa hao wanatarajia kuhamia katika makazi yao mapepya hivi karibuni baada ya kumaliza muda wao katika jumba walilopanga huko Malibu kwa ajili ya mapumziko na watoto wao mapacha ambao wamezaliwa hivi karibuni.

Mwezi April mwaka huu, Jay na Queen Bey walitajwa kutaka kununua mjengo mpya uliopo Mashariki mwa mji wa Los Angeles ambao ulikuwa na thamani ya dola miioni 130. Habari njema ni kuwa mastaa hao tayari wamefanikiwa kuubeba mjengo huo kwa kiasi cha dola milioni 120.

Nyumba hiyo ina eneo lenye ukubwa wa sentimita za mraba 30,000, vyumba vinane vya kulala, mabafu 11, mabwawa ya kuogelea manne, studio ya kurekodia muziki, uwanja wa kuchezea mpira wa kikapu, uwanja wa kuchezea tennis na vingine.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents