Picha: Kampeni ya kutokomeza Malaria kwa kutumia simu za mkononi yazinduliwa jijini Dar
Malaria No More, ikishirikiana na Tanzania House of Talent na Vodacom Foundation Jumatano hii imefanya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini kwa kutumia simu za mkononi. Uzinduzi huo umefanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo itaangalia jinsi teknolojia ya simu inavyoweza kutumiwa kiubunifu kuzungumzia masuala ya afya ya jamii kama Malaria.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal pamoja na Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal akizungumza katika uzinduzi huo
Dkt Bilal alisema amependa kuona wasanii wa muziki wanatumia uwepo wao katika jamii kwa kufundisha na kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali.
“Niwashukuru wasanii kwa kuendelea kupeleka ujumbe wakuelimisha kwa jamii, mnafanya kazi mzuri sana,na muziki unakuwa kwa kasi sana kuliko nchi nyingine,” alisema Dkt Bilal.
Pia Dkt Bilal alisema anawashukuru Vodacom kwa kuendelea kusaidia mambo muhimu nchini na pia kwa kuunda mfumo wa simu ambao utawawezesha Watanzania kupata taarifa za malaria. Aidha amewaomba Vodacom waendelee kusaidia ili taifa liendelee kukua.
Kwa upande wake Dkt Hussein Ali Mwinyi alisema serikali inatambua jitihada za mashirika mbalimbali katika kupambana na malaria nchini na kuongeza kuwa takwimu zinaonyesha jitihada za serikali zikishirikana na za mashirikika mbalimbali wameweza kupunguza vifo vya ugonjwa wa malaria.
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika uzinduzi huo
Picha ya pamoja wa viongozi pamoja na wadau waanzilishi wa kampeni ya kutokomeza malaria
Katika kampeni hiyo, wananchi watakuwa na uwezo wa kutumia simu kufahamu taarifa mbalimbali kuhusiana na kujikinga na Malaria kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu, robo-calls na IVR (Interactive Voice Response). Ujumbe unaohusiana na Malaria utakuwa ukiwasilishwa na watu mashuhuri nchini akiwemo Rais Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa na Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mwakilishi kutoka THT, Ruge Mutahaba alisema wasanii watakuwa wakiimba nyimbo za kuhamasisha Watanzania njia mbalimbali za kujikinga na ugonjwa wa malaria kwakuwa wasanii hao wanap mashabiki wengi na kioo cha jamii hivyo kupitia wao ujumbe utafika kwa urahisi na kusaidia kutokomeza kwa kasi ugonjwa huo.
Ruge Mutahaba akiongea katika uzinduzi huo
“Wasanii wanaweza wakawa mabalozi wakubwa sana katika kufikisha ujumbe wa kupambana na malaria kwa jamii hivyo tuliona tukiwatumia tutafanikiwa kutokemeza malaria kwa kiasi kikubwa sana,” alisema Ruge.
Vijana toka THT wakitoa burudani kwenye uzinduzi huo
Amini na Barnaba wakiimba kwa tabasamu
Msanii Barnaba akipeana mkono na Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal
Ben Pol akipeana mkono na Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal
Linah,Racho, Barnaba na Amini wakitoa burudani
Kushoto msanii wa muziki toka THT Asia akiwa na rafiki yake
Mwakilishi kutoka Malaria No More Lilian akiongea katika uzinduzi huo
Ruge akiteta jambo na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi huo