Burudani

Picha: Kanisa lenye umbo la kiatu cha kike (high heels) lajengwa Taiwan

Kanisa lenye urefu wa mita 16 lililojengwa kwa kutumia vioo linalofanana na viatu vya kike vyenye visigino virefu (high heels) limejengwa huko Taiwan kwa lengo la kuwavutia wanawake zaidi.

kanisa kiatu-1

Kanisa hilo limetengezwa na maafisa wa baraza la miji kusini magharibi mwa pwani, katika eneo moja la kitalii lenya umaarufu mkubwa huko Taiwan.

kanisa kiatu-3

Kwa mujibu wa BBC, ujenzi wa kanisa hilo umechukua miezi miwili na umegharimu dola 686,000 sawa na zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne.

kanisa kiatu-2

Pan Tsuei-ping, msimamizi wa ujenzi huo, ameiambia BBC kwamba kanisa hilo litakuwa likitumika zaidi kwa matumizi ya hafla za harusi na kupiga picha, halitatumika kwa ibada za kawaida za kila siku.

Kanisa hilo litafunguliwa rasmi tarehe 8 mwezi Februari 8, lakini hadi sasa limekuwa kivutio kikubwa kwa watu ambao wamekuwa wakijitokeza kupiga picha mbele yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents