Aisee DSTV!
SwahiliFix

Picha: Kidoti ya Jokate Mwegelo yaingia ubia na kampuni ya China

Brand ya urembo, Kidoti iliyoanzishwa na mtangazaji wa TV nchini, Jokate Mwegelo, imeingia mkataba na kampuni ya Rainbow Shell Craft ya nchini China.

Jokate na Mr Deng wakisaini mkataba
Jokate na Mr Deng wakisaini mkataba

Jokate ameiambia Bongo5 kuwa mkataba huo una gharama ya shilingi bilioni 8.5. “Tutajenga viwanda, kufungua maduka. Kuiweka Kidoti kama brand namba moja nchini na kwingine,” amesema. Wamewekeza kiasi hicho cha fedha ili kuliwezesha hilo na pengine mengi zaidi. Ni kitu cha kunufuika sote.”

Kampuni hiyo inamiliki viwanda vya nywele na bidhaa zingine za urembo.

4K0A5391

Jokate na kampuni hiyo imesaini mkataba huo wa ubia Ijumaa hii kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Jokate akiongea na waandishi wa habari
Jokate akiongea na waandishi wa habari

“Ubia huu unalenga kuiwezesha Kidoti kuweza kupanua wigo wake kibiashara ikitazama kujiweka zaidi katika soko la Afrika Mashariki na kati na kuendelea kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi,” alisema Jokate.

4K0A5369

Aliongeza kuwa ubia huo utawezesha kujengwa viwanda nchini vitakavyotoa fursa ya ajira.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Rainbow Shell Craft, Mr. Deng alisema kuwa katika kipindi kifupi kijacho, Kidoti itakuwa brand kubwa Afrika Mashariki.

Jokate na Mr Deng baada ya kusaini mkataba
Jokate na Mr Deng baada ya kusaini mkataba

“Kampuni ya Kidoti imeingia ubia na Rainbow hapa Tanzania ili iweze kuwa bidhaa bora na kuyependeza zaidi,” alisema.

Jokate amesema bidhaa za Kidoti zinabuniwa na wabunifu wa Kitanzania wa kampuni hiyo na Rainbow ikitengeneza kile kilichobuniwa na kwamba tayari zinapatikana kwenye supermarkert za Uchumi.

“Mpango ni kuzifanya zianze kupatikana kwenye soko la Kariakoo ambako tunaamini itakuwa rahisi kwa wananchi wengi kuzipata,” alisema Jokate.

Hizi ni picha zaidi.

Baadhi ya bidhaa mpya za Kidoti
Baadhi ya bidhaa mpya za Kidoti

Baadhi ya warembo waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya warembo waliohudhuria mkutano huo

Baadhi ya wawakilishi wa China waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya wawakilishi wa China waliohudhuria mkutano huo

Jokate akielezea bidhaa mpya za Kidoti
Jokate akielezea bidhaa mpya za Kidoti

Jokate Mwegelo na Mr Deng wakijiandaa kusaini mkataba wa ubia
Jokate Mwegelo na Mr Deng wakijiandaa kusaini mkataba wa ubia

Jokate na Mr Deng wakisaini mkataba
Jokate na Mr Deng wakisaini mkataba

Mbunge wa Viti Maalum Dar es Salaam, Mariam Kisangi
Mbunge wa Viti Maalum Dar es Salaam, Mariam Kisangi

Meya wa Manispaa Ilala, Jerry Slaa akiongea na waandishi wa habari
Meya wa Manispaa Ilala, Jerry Slaa akiongea na waandishi wa habari

Mshereheshaji kwenye mkutano huo, Ezden Jumanne
Mshereheshaji kwenye mkutano huo, Ezden Jumanne

Mwenyekiti Mtendaji wa uwakilishi wa kibiashara wa kiuchumi na kibiashara kati ya serikali za  China na Tanzania, Mr Lin
Mwenyekiti Mtendaji wa uwakilishi wa kibiashara wa kiuchumi na kibiashara kati ya serikali za China na Tanzania, Mr Lin

Ndala ni miongoni mwa bidhaa mpya za Kidoti
Ndala ni miongoni mwa bidhaa mpya za Kidoti

Picha ya pamoja baada ya shughuli ya kusaini mkataba wa ubia kumalizika
Picha ya pamoja baada ya shughuli ya kusaini mkataba wa ubia kumalizika

4K0A5391

4K0A5395

4K0A5405

4K0A5410

4K0A5444

4K0A5456

4K0A5466

4K0A5487

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW