Burudani

Picha: Kidumu alivyowasha moto Sauti za Busara

Usiku wa kuamkia leo msanii wa muziki ambaye ni mzaliwa wa Burundi anayeishi nchini Kenya Kidumu, ameweza kukonga nyoyo za mashabiki wake katika tamasha lamuziki la Sauti za Busara liliofunguliwa rasmi kwa gwaride hapo jana.

Kidumu akiambatana na band yake ya The Boda Boda Band waliweza kutoa burudani ya aina yake kwa wapenzi wa muziki na wapenzi wa tamasha hilo waliojitokeza Ngome Kongwe kisiwani Zanzibar.

Nyimbo zilizotumika kupamba jukwaa ni ‘Kichuna’,’Haturudi Nyuma’ aliyofanya na Juliana kutoka Uganda, ‘Nitafanya’ aliyoimba na Lady Jaydee kutoka Tanzania na nyinginezo zinazofanya vizuri Afrika na Ukanda wa Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents