Picha

Picha: Kifo cha Aaliyah chatimiza miaka 12 jana

Hollywood ilimpoteza staa wa R&B, Aaliyah miaka 12 iliyopita. Muimbaji huyo mzaliwa wa Brooklyn, alipoteza maisha kwenye ajali ya ndege Aug. 25, 2001. Alikuwa akitokea kwenye visiwa vya Bahamas, ambako alienda kushoot video ya wimbo wake “Rock The Boat”. Alikuwa na miaka 22 tu.

Sean "P. Diddy" Combs Independence Day Softball Game and BBQ

Aaliyah alianza kung’ara akiwa na umri mdogo. Alionekana kwenye show ya Star Search akiwa na miaka 10 na kisha kusainiwa na Jive Records miaka miwili baadaye.

R&B singer Aaliyah and hip-hop mogul Damon Dash are on hand
Aaliyah na Damon Dash

R. Kelly alikuja kuwa mwalimu wake katika kipindi cha mwanzo cha career ya muziki ya Aaliyah. Alikuwa na vipaji vingi na kupitia muziki aliweza kutengeneza hits kibao “Are You That Somebody” na “Try Again.”

2001 MTV Movie Awards - Backstage
Aaliyah akiwa na Destiny’s Child

Pia alifanya vizuri kwenye filamu kwa kuigiza kwenye “Romeo Must Die” na “Queen of the Damned.”

Romeo Must Die

Queen Of The Damned

Hadi sasa sauti yake bado inaendelea kutumiwa na wasanii wapya wakiwemo Drake na Chris Brown.

Atakumbukwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents