Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Picha: Kijana afikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya mtu asiyejulikana

Kijana Salum Nkonja(22), Mkazi wa Ipililo wilayani Maswa, Shinyanga, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo akikabiliwa na kosa la mauaji ya mtu asiye fahamika.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika kijana huyo alikamatwa katika kituo cha mabasi cha Ubungo kilichopo jijini Dar es salaam akiwa na viungo vya binadamu ambazo ni sehemu mbalimbali za mwili wa mwanamke ambazo hazijafahamika na nyara za serikali.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha. Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 8 Disemba mwaka huu, upelelezi bado haujakamilika.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW