Habari

Picha: Kijana ashangaza dunia kwa kupanda mwamba mgumu zaidi kwa muda mfupi

By  | 

Adam Ondra ambaye ni raia wa Jamuhuri ya Czech, amefanikiwa kujitengenezea rekodi mpya duniani katika ukweaji wa miamba.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, alijitengenezea rekodi hiyo kwa kupanda mja ya mwamba mkubwa na mgumu uliopo nchini Norway kwa dakika ishirini baada ya kufanya mazoezi ya kupanda mwamba huo kwa tajkribani miaka miwili.

Akiongea na Newsbeat, Adam amesema, “Nilipojua nilifanya hivyo, nilikuwa na hisia ya ajabu sana. Sikuweza hata kupiga kelele. Yote niliyoweza kufanya ilikuwa tu kwenye kamba, nihisi machozi machoni mwangu. Ilikuwa furaha kubwa. Miezi na miezi ya maisha yangu yalihitimishwa kwa dakika 20.”

Mwamba huo unaopatikana katika maeneo ya Flatanger, hutajwa na wakweaji wengi kama ni mmoja ya mwamba mgumu zaidi duniani katika kuupanda.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments