Habari

Picha: Kijana wa Kimasai afunga ndoa ya kifahari, avuta majiko mawili kwa wakati mmoja

Morani mmoja katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya ameacha watu midomo wazi baada ya kufunga ndoa ya kifahari kwa kuowa wanawake wawili kwa mpigo.

Tom Matiko

Tom Mako, maarufu kama Junior, 27, alifanya sherehe hiyo ya harusi Jumanne wiki hii.

Mako anatokea kwenye familia ambayo ndoa za wake wengi ama mitala ni jambo la kawaida.

Hata hivyo kuoa wake wawili kwa mpigo ni jambo ambalo halikuwahi kusikika katika jamii ya Kimaasai ambayo wanandoa hao wametokea. Wapo wanaume wanaowaoa wake wengi lakini si kwa wakati mmoja.

Harusi

Katika harusi hiyo ambayo ilipambwa vilivyo katika kitongoji cha Kisaju, Mako aliwaoa Elizabeth Silamoi, 25, na Joyce Tikoyian, 23.

Harusi hiyo imeonekana kama ya kifahari hasa kulingana na tamaduni za Wamasai zilivyo, kwani mama bibi harusi walivalia mashela na kurembwa vizuri wakati bwana harusi akivalia suti na kuondoka kupitia usafiri wa gari maalum ambayo ilikuwa imeandaliwa baada ya ndoa hiyo kupita.

Wote wawili ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenya Assemblies of God mjini Kitengela, si mbali sana na eneo Kisaju anakoishi Tom.

Huhudhuria masomo na kurejea nyumbani jioni. Wamekuwa pamoja kwa mwaka mmoja, na sherehe ya Jumanne ilikuwa ya kurasmisha ndoa kati ya kitamaduni.

Harusi

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mako alikutana na Bi Silamoi miaka miwili iliyopita wakati akichunga ng’ombe wake karibu na nyumabni kwa mwanamke huyo.

Mwaka jana akakutana na Bi Tikoyian pia akiwa anachunga ng’ombe karibu na kwao.

Katika mila za Kimasai, mahari ya ng’ombe hutolewa kabla ya kufungwa kwa ndoa, na bwana harusi Mako alikamilisha hilo ipasavyo.

Mako aliwaoa wakeze kimila japo wote walivalia mavazi ya kimagharibi. Mako alivalia suti ya rangi ya samawati na wakeze wakivaa mashela meupe. Wote pia walivalia urembo wa Kimaasai.

“Nataka kuliweka sawa hili, harusi yangu ilikuwa ya kimila na haikuwa na mahusiano yoyote na kanisa. Kuna watu wanatuma habari za kupotosha mitandaoni kuwa ndoa yangu ilisimamiwa na wachungaji,” Mako, ambaye ni mfanyabiashara, amenukuliwa na gazeti la kibinafsi la Star la nchini Kenya.

Amesema amewaoa wanawake hao kwa sababu wote wanampenda na hakutaka kumsononesha yeyote kati yao.

Waliohudhuria

“Huu ni ujumbe ninaoutuma kwa waume wa kisasa wanaojifanya kuwa wanampenda mwanamke mmoja na huku wakiwalaghai kwa kuingia kwenye mahusiano na wengine pembeni,” amesema na kuongeza:”Nimekuwa muaminifu kwa wake zangu kwa sababu sitakuwa na sababu ya kuongeza mke mwengine. Ninaamini wawili watanitosheleza.”

Keki 2

Bi Silamoi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye penzi na Mako, na kusema kabla ya kuja kwa mwenzake wawili hao walijadiliana kwa kina na kukubaliana.

“Ninampenda. Nilimpa Baraka zangu kuongeza mpenzi. Nampenda (mke mwenzake) pia.”

Bi Tikoyian, amesama wote wamekubaliana kuwa katika mahusiano ya aina hiyo na wazazi wake walikubali hilo kwa sababu wanamuamini Mako.

Bi Silamoi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye penzi na Mako, na kusema kabla ya kuja kwa mwenzake wawili hao walijadiliana kwa kina na kukubaliana.

“Ninampenda. Nilimpa Baraka zangu kuongeza mpenzi. Nampenda (mke mwenzake) pia.”

Bi Tikoyian, amesama wote wamekubaliana kuwa katika mahusiano ya aina hiyo na wazazi wake walikubali hilo kwa sababu wanamuamini Mako.

Harusi

Wazazi wa bwana harusi,Bw Mako Busabus na Bi Sintiyio, wamesema hawakuamini mwanzoni mtoto wao alipowaambia anataka kuoa wake wawili kwa siku moja, na sherehe moja. Lakini hilo limepita.

“Kwa umri wangu wa miaka 90 sijawahi kuona kitu kama hiki huku umasaini. Kwa kawaida, mtu anayetaka kuongeza mke husubiri kwanza walau baada ya mwaka au miaka miwili toka alipofunga ndoa ya kwanza,” amesema Busabus.

Harusi

Mamorani wengine pamoja na wageni waliohudhuria harusi hiyo wanamchukulia Mkako kama shujaa kwa kufanya jambo ambalo halikuwahi kufanyika kabla umasaini.

Harusi

Harusi

Mawaidha

Baada ya harusi, watatu hao wamekuwa wakiendelea na maisha yao.

Hapa wanaonekana wakiwa mtaani kwao Alhamisi

Hapa wanaonekana wakiwa myumbani kwao Alhamisi

Wakiwa nyumbani kwao Alhamisi

Wakiwa nyumbani kwao Alhamisi

Ingawa Bi Silamoi na Bi Tikoyian wanatokea ukoo mmoja, hawajatokea familia moja.

Bi Silamoi (kushoto) na mke mwenza wake Bi Tikoyian

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents