DStv Inogilee!

Picha: Kim Jong-un alivyofanya ziara yake ya kwanza duniani na kukutana na Rais Xi Jinping

Ukweli umefahamika kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amefanya ziara nchini China baada ya tetesi za uvumi huo kusambaa kila kona.                Kim Jong-un (kushoto) akiwa na Rais Xi Jinping

China na Korea Kaskazini wamethibitisha ziara hiyo ya Kim Jong-un ambapo amekutana na Rais Xi Jinping mjini Beijing.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliwasili katika eneo hilo kwa treni ya kijeshi huku kukiwa na ulinzi mkali uliowekwa kwenye maeneo ya mji wa Beijing.

Kim Jong-un akishuka kwenye treni na kupokelewa na viongozi wa ngazi za juu wa China

Hiyo ni ziara ya kanza kwa Kim Jong-un nje ya taifa la Korea Kaskazini tangu alipochukua madaraka mwaka 2011. Wakati huo huo imedaiwa kuwa kwa mwaka huu kiongozi huyo atakutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi April na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW