Habari

Picha: Kimbunga cha Sandy kilivyoiacha ‘taaban’ pwani ya Mashariki ya Marekani

Tufani (Kimbunga) ya Sandy iliyoikumba pwani ya Mashariki ya Marekani hususan katika majiji ya New York na New Jersey, imeacha hasara kubwa.

Licha ya kusababisha vifo vya takriban watu 40, kimbunga hicho kimesababisha hasara ya zaidi ya dola bilioni 20 huku dola bilioni 10 hadi 30 zikiwa za biashara zilizoharibika, kwa mujibu wa shirika la IHS Global Insight.

Dhoruba hilo limeyakosesha huduma ya umeme makazi zaidi ya milioni 7 huku likiharibu asilimia 70 ya maghala ya pwani ya Mashariki.

Safari za meli zimesimama kwa muda katika maeneo mengi na pia ndege zaidi ya 15,000 katika eneo hilo la kaskazini mashariki zimeshindwa kufanya safari hivyo kuwafanya wasafiri kukaa siku kadhaa bila kwenda walikotaka kwenda.

Jana zaidi ya ndege 6,000 zilishindwa kusafiri na pia safari 500 za ndege leo zimesitishwa.Viwanja vikubwa vitatu vya New York vilifungwa jana.

Jiji la New York ndilo lenye shughuli nyingi zaidi za ndege nchini Marekani hivyo kusitishwa kwa safari hizo kutakuwa na athari kubwa za kiusafiri kwa majiji mengine.

Sandy imeingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa miongoni mwa vimbunga 10 vilivyosababisha hasara zaidi nchini Marekani.

Hata hivyo Hurricane Katrina ilikuwa mbaya zaidi kwani ilisababisha hasara ya dola bilioni 108 na kusababisha watu 1,200 kupoteza maisha mwaka 2008.

Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha madhara ya kimbunga cha Sandy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents