Habari

Picha: Kiumbe huyu wa ajabu apewa jina la Donald Trump, haoni na anaishi majini na nchi kavu

Kiumbe anayeweza kuishi baharini na katika nchi kavu amepewa jina la Rais wa Marekani Donald Trump, ingawa huenda kiongozi huyo asitake kuhusishwa na kiumbe huyo kutokana na sifa zake.

Composite image showing the Dermophis donaldtrumpi with photoshopped hair, and US President Donald Trump

Amfibia huyo huwa anafukia na kuficha kichwa chake mchangani anapokabiliwa na hatari, jambo ambalo pengine limewashawishi wahusika kumpa kiumbe huyo jina la Trump kutokana na kiongozi huyo kukana kwamba shughuli za viwanda na za kibinadamu zinachangia mabadiliko ya tabia nchi. Kiumbe huyo pia ni kipofu, hawezi kuona.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC,The Guardian , The Nation na vyombo mbalimbali vya habari, Mnyama huyo ambaye amepewa jina Dermophis donaldtrumpi, aligunduliwa katika eneo la Panama, na alipewa jina hilo na mkuu wa kampuni ya EnviroBuild ambaye alikuwa amelipa $25,000 (£19,800) kwenye mnada kupata fursa ya kumpa jina kiumbe huyo.

Kampuni hiyo imesema inataka kuhamasisha watu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

“[Dermophis donaldtrumpi] huathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi na kwa hivyo ni kiumbe aliye katika hatari ya moja kwa moja ya kuangamia kutokana na sera ya somo wake kuhusu mazingira,” mwanzilishi mwenza wa EnviroBuild, Aidan Bell, amesema kupitia taarifa.

Dermophis donaldtrumpi

EnviroBuild, kampuni iliyopata haki yakumpa kiumbe huyo jina, iliongeza nywele bandia kwenye kiumbe huyo jambo lililomfanya kuwa na muonekano unaokaribiana na wa Trump

Kiumbe huyo mdogo ni wa aina ya caecilian, ambao ni viumbe watelezi wanaofanana na minyoo au nyoka, na huishi sana chini ya ardhi.

Bw Bell amesema tabia za kiumbe huyo zinashabihiana sana na za Trump.

“Kupuuza mambo (sawa na kuficha kichwa mchangani) humsaidia Donald Trump kukwepa maafikiano kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabia nchi,” amesema.

The Dermophis donaldtrumpi, which was discovered in Panama

Pesa zilizopatikana kutokana na kupiga mnada nafasi ya kumpa kiumbe huyo jina zitakabidhiwa shirika la Rainforest Trust

Wanasayansi duniani wanakubaliana kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na shughuli za kibinadamu.

Lakini Bw Trump, ambaye utawala wake umekuwa ukiendeleza matumizi ya mafuta yanayotokana na kaboni, amewatuhumu wanasayansi hao kwa kuwa na “ajenda ya kisiasa” na kutilia shaka kwamba binadamu wanahusika katika ongezeko la joto duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents