Picha

Picha: Kondakta mzungu mwanamke kwenye matatu, ‘sista duu’ wa bongo anaweza?

AY alishawahi kuimba “jaribu hii, kavae ndala na mzungu akavae ndala muongozane hoteli kubwa ye atapita we utapigwa mkwara”! Yes! nimeukumbuka huo mstari kwa haraka baada ya kukutana na picha hii ya msichana wa kizungu ambaye ameonekana katika matatu (daladala) akipiga kazi ya ukondakta huko Kenya.

kondakta mzungu

Well, watu wengi huwa wanaamini kuwa kuna kazi flani zipo kwaajili ya watu wa hali ya chini na zingine kwaajili ya watu flani wa hali ya juu, na mtu mweupe anaaminika kuwa hawezi kufanya aina flani ya kazi ‘eti’ kwasababu ni ‘white’.

Hiyo picha ni ya mzungu tena msichana mrembo tu ambaye anapiga kazi ya ukondakta katika matatu huko Kenya ambazo hapa kwetu tunaita daladala. Je yule ‘sista duu’ unayeweza kukutana naye Cinemax mlimani City anaweza??

Kazi ni kazi tusidharau kazi ili mradi inakuletea uji,vitumbua, viazi, sausage, burger,mezani!

Kama nilivyoanza, namaliza na mstari mwingine wa AY “inategemea na mtu, si kila unaemwona kimavazi unamdharau tu na wakati wako safi tu halafu wako simple tu kwani mavazi kuvaa ni uamuzi wa mtu”, unaweza kugeuza maana ya huo mstari kwenye upande wa kazi!

Picha: Kenyan post

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents