Habari

Picha: Kongamano la ‘Her Initiative’ lafana UDSM

Leo Jumamosi ya Mei 13, kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limefanyika kongamano la awamu ya tatu la ‘Her Initiative’ linalosaidia kuwaelimisha watoto wa kike kujitambua na kuwa wajasiriamali.

Kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya HER INITIATIVE lilihudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam na wasichana wajasiriamali pamoja na wageni kadhaa wakiwemo, Faraja Nyalandu, Martin Kadinda, Jokate Mwegelo, Elizabeth Muro na Makoye Philbert ambaye ni muuzaji wa Mike Juice.

Akiongea na watu waliohudhuria kwenye kongamano hilo, Faraja Nyalandu ambaye ni mkurugenzi na muasisi wa taasisi ya Shule Direct, amewataka wanafunzi hao kuweza kuwa na nidhamu ya kujiwekea katika maisha yao. “Ukipata laki moja badala ya hela yote kwenda kununulia wigi, basi hela hiyo wekeza katika biashara. Ukisikia usingizi usilale pambana na kufanya kazi, hiyo ndio nidhamu. Badala ya kwenda kukesha klabu usiku basil ala ili ukiamka asubuhi uwe na nguvu ya kwenda kufanya kazi kwa bidii,” amesema Nyalandu.


Mkurugenzi na mwanzilishi wa taasisi ya Shule Direct, Faraja Nyalandu akiongea kwenye kongamano la Her Initiative, UDSM

Miss huyo wa Tanzania 2004 amewasisitiza wajasiriamali hao, kuweza kujidhamini wenyewe kabla ya kudhaminiwa na watu wengine ndipo hapo wataona dhamani yao kama ilivyo kwa Orpah Gail Winfre na Beyonce pamoja na mastaa wengine.

Naye Martin Kadinda amewaambia wasichana hao wanatakiwa kuwa tofauti na mtu mwengine kaika maisha, kujichukulia kama yatima kwenye maisha hivyo itaweza kusaidia watu kusaidiana pamoja na kuwa na upendo kwa kila mmoja.


Martin Kadinda akitoa neno mbele ya wanafunzi, UDSM

Kwa upande wake Jokate, amewataka wanafunzi hao kuiga ujasiri kama aliokuwa nao mwanzilishi wa taasisi ya HER INITIATIVE na mtangazaji wa Fema Tv na radio shows, Lydia Charles. Mwegelo amemtaja mrembo huyo kuwa ni mpambanaji wa aina yake na anajitolea zaidi kwa ajili ya wasichana wenzake japo amekuwa na maradhi ya moyo ambayo yangeweza kumkatisha tamaa.

Aidha Elizabeth Muro ambaye ni company secretary and counsellor wa Commercial Bank of Africa, CBA, amewataka wanafunzi hao wasikubali kukatishwa tamaa kutokana na changamoto wanazozipata kwani hata yeye kufikia hapo alipo aliwahi kuambiwa na bosi wake kuwa yeye ni kama Kindergarten Lawyer kukalia kiti hicho ambacho aliiomba nafasi hiyo kutokana na bosi aliyekuwa akikalia kiti hicho alipoamua kuondoka.


Elizabeth Muro, wakwanza kulia akiwa katika kongamano hilo UDSM

Naye Makoye Philbert ambaye ni muuzaji na mmiliki wa Mike Juice, amewataka wasichana hao kutokata tamaa kwenye maisha japo kumekuwa na vikwazo vingi. Mike ametolea mfano wa maisha yake ambapo amesema alianza kazi katika kampuni ya Vodacom kwa kulipwa mshahara wa laki mbili kwa mwezi pamoja na kukumbana na changamoto nyingi za kimaisha hali iliyompelerkea mpaka kuuza vitu vyake vya ndani, lakini mpaka sasa amewaajiri wafanyakazi saba na anawalipa mshahara wa wastani wa shilingi laki tatu kwa mwezi kila mmoja.


Muuzaji na mmiliki wa Mike Juice akitoa neno kwenye komngamano la Her Initiative

Wakati huo huo taasisi hiyo imemtangaza Maureen Richard kuwa Mwenyekiti wake mpya huku Irene Enock aliyekuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa taasisi hiyo akistaafu baada ya kutekeleza majukumu yake katika kipindi chake cha takriban miezi sita tangu alipotangazwa kukalia kiti hicho Novemba 26 ya mwaka jana.


Maureen Richard ambaye ni mwenyekiti mpya wa taasisi ya Her Initiative


Lilian Masuka wa kwanza kushoto akimkabidhi begi la ‘Kidoti’ Nickson George wa Clouds na wamwisho kulia ni Meena Ally wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM


Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala akiwa na mmoja ya wafanyakazi kutoka taasisi ya Shule Direct

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents