Habari

Picha: Kundi la muziki laamua kulima mahindi na mboga mboga ndani ya studio ya kurekodi muziki huku wakirekodi album yao!!

Katika miji iliyoendelea hasa maeneo ya mijini ambapo hakuna maeneo ya kufanya kilimo watu wamekuwa wakilima mazao mbalimbali ndani ya nyumba zao na kuwawezesha kupata chakula na matunda kutoka katika mazao hayo ambayo hulimwa kisasa zaidi.

shamba la ndani-4
Shamba la mahindi la ndani la kundi Limp Bizkit

Kundi la kimarekani la Limp Bizkit nao wameamua kulima shamba la ndani ya nyumba “a micro-indoor farm” ambalo lina mazao ya mahindi na mboga mboga. Kwa mujibu wa TMZ Kundi hilo ambalo linarekodi album yao mpya ya “The Paradigm Shift” limeamua kufanya hivyo ili wasipate tabu baadae ya kwenda kununua supermarket.

Kilimo cha ndani hufanywa kwa kupanda mbegu za mazao katika vyombo maalum ndani ya nyumba kwa kufuata maelekezo ya kitaalam kama inavyoonekana katika baadhi ya picha hapo chini.

shamba la ndani-1

shamba la ndani-3

shamba-5

shamba-6

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents