Picha kutoka msibani kwa Bi. Kidude, Zanzibar
Baada watanzania na dunia nzima kupokea taarifa ya kifo cha msanii mkongwe wa taarabu asilia, Bi. Kidude, jana Bongo5 ilifunga safari kuenda eneo la Raha Leo, kisiwani Zanzibar ambako alikuwa akiishi Marehemu.
Bi. Kidude anatarajiwa kuzikwa na wadau mbalimbali kutoka kila kona ya dunia.Ikiwa katika eneo la tukio, imeongea na mjukuu mlezi wa Bi. Kidude, Omary ambaye alieleza ratiba ya mazishi na vilevile kilichosababisha kifo chake jana saa 7 mchana.
Omary amesema “Marehemu amefariki jana mchana nilipigiwa simu nikaambiwa hali ya mgojwa ni mbaya, na kweli nilifika nikamkuta hali yake haikuWa nzuri mpaka saa 7 mchana alivyotutoka.”
Bi. Kidude alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya tumbo kama uvimbe, na pia alikuwa na kisukari.
“Marehemu atazikwa Kitumba ambapo ndipo chimbuko la baba yake mzazi. Mazishi yataanza saa 7 mchana na kuendelea kutokana na watu wengi kuWa mbali na kuhitaji kuhudhuria.