Habari

Picha: Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yalivyofanyika katika Viwanja vya JK Youth Park

Ijumaa hii ya Juni 16 ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika ambapo kwa jiji la Dar es Salaam maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Yourth Park maeneo ya Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja.

Katika sherehe hizo mgeni rasmi alikuwa ni Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Roeland Van de Geer, ambaye pia aliweza kukagua gwaride lililoandaliwa na watoto kutoka Shule ya Tandika pamoja na kushuhudia burudani nzito iliyotolewa na watoto wenye umri wa takriban miaka miwili mpaka mitatu kutoka kwenye taasisi ya Beginners Foundation.


Picha ya mgeni rasmi, Balozi Roeland Van de Geer (Wa pili kutoka kushoto)

Wakati huo huo katika maadhimisho hayo watoto kutoka shule mbalimbali walihudhurika katika maaadhimisho hayo ambayo yalipambwa na utoaji wa elimu kwa watoto hao kutoka kwa taasisi mbalimbali ikiwemo Jenga Hub, ambayo inawafundisha watoto elimu ya teknolojia ikiwemo kutumia computer.

Hizi ni picha nyingine za maadhimisho hayo.


Mgeni rasmi akikagua gwaide lililoabdaliwa na wanafunzi kutoka Tandika


Watoto kutoka Beginners Foundation wakisubiri kutoa burudani kwa watu


Mtoto akiwa katika banda la Jenga Hub akipewa elimu ya teknolojia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents