Michezo

Picha: Maelfu ya wanasoka wajitokeza kuuwaga mwili wa Regis

Mashabiki na wapenzi wa soka wamejitokeza kwa wingi katika mitaa mbalimbali kuuwaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa klabu ya West Brom na timu ya taifa ya England, Cyrille Regis.

Maelfu ya watu wamejitokeza katika makao makuu ya klabu ya West Brom kutoa heshima zao za mwisho.   Meneja, Alan Pardew ameiongoza timu yake na baadhi ya wafanyakazi wa klabu hiyo nje ya makao makuu yao.

Regis,alifariki ghafla Januari 14 ya mwaka huu anachukuliwa kama mmoja wa wachezaji wa kukumbukwa katika historia ya mchezo wa soka.

Wachezaji wa West Bromwich Albion akiwemo Gareth Barry (watatu kutoka kulia), akijumuika katika maombolezo hayo

Cyrille Regis amezaliwa February 9 mwaka 1958 na umauti umemfika January 14 mwaka  2018, katika maisha yake ya soka amecheza nafasi ya ushambuliaji ndani ya timu ya taifa ya England kwa muda wa miaka 19 wakati akifanikiwa kucheza michezo 614 na kushinda magoli  158 na kushinda vikombe vitano akiwa na timu yake ya taifa.

Meneja wa West Bromwich Albion, Alan Pardew akiwa na wachezaji wake na baadhi ya wafanya kazi wakitoa heshima zao za mwisho katika mwili wa, Cyrille Regis

Meneja, Alan Pardew akiiongoza timu yake na wafanyakazi nje ya klabu

Mourner akitoa heshima zake za mwisho kwa  Cyrille Regis nje ya uwanja wa West Midlands

Regis akiwa mchezaji mweusi ndani ya timu ya taifa ya English amecheza michezo 297 na kutupia mabao 112

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents