Habari

Picha: Mafuriko yaufunika mji wa Edgecumbe nchini New Zealand

Maelfu ya watu wanaoishi katika mji wa Edgecumbe uliopo kaskazini mwa nchi ya New Zealand wameyakimbia makazi yao baada ya mafuriko makubwa yaliyozunguka mji huo kutokana na mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga cha Debbie.

Kimbuka hicho pia kiliiathiri nchi ya Australia Alhamisi ya wiki iliyopita na kusababisha mito mbalimbali katika nchi hiyo kujaa kingo zake.

Katika mji wa Edgecumbe maji yanasemekana kufika hadi mita 2 katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo hakuna ripoti yoyote ya kifo katika mafuriko hayo lakini kuna mtu mmoja ambaye alikuwa katika mto ndio anatafutwa na mpaka sasa hajaonekana.

Polisi katika mji huo wamesema watapiga doria katika maeneo yaliyohamwa na kuweka vizuizi kuwazuia raia wasije wakarudi. Tazama picha za mafuriko katika mji huo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents