Picha: Maji ya simamisha ujenzi uwanja wa Tottenham Hotspur
Ujenzi wa uwanja mpya wa klabu ya Tottenham Hotspur ulisimama kwa muda mwishoni mwa juma hili kufuatia kupasuka kwa ‘pipe’ kubwa iliyotiririsha maji kwa zaidi ya dakika 45 yaliyoelekea kwenye miundombinu ya umeme.
Mamia ya lita za maji yalimwagika siku ya Ijumaa na kufanya kusimama kwa ujenzi wa uwanja huo uliyogharimu mamilioni ya fedha wakati uzinduzi wake ukikusudiwa kufanyika mwezi Oktoba.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 8.45 asubuhi siku ya Ijumaa na kupelekea wafanyakazi kuhaha katika kuhakikisha wanazuia tatizo hilo.
Chanzo kimoja cha habari kimesema kuwa maji mengi yalimwagika baada ya ‘pipe’ kubwa ya maji kupasuka wakati watu wakiwa wanafanyakazi.
Na kusisitiza kuwa mabosi wote wanaowasimamia wafanyakazi walilazimika kushuka chini sehemu ya kiwanja ili kuhakikisha wanalizuia tatizo hilo huku maji hayo yakionekana kusambaa kwenye miundombinu ya umeme.
Mapema mwezi huu, Spurs ilitangaza kuwa mpaka mwezi wa Oktoba Tottenham Hotspur itahamia kwenye uwanja wake mpya.
Shkamoo mvua
Hawa jamaa wamejipanga hata hvyo hiko kiwanja sio mchezo….sio hapa Tz uwanja eti ulikosewa raman bas jua kama lote vile…..tatzo bongo siasa nying ktk mambo ya michzo