Habari

Picha: Mamia wajitokeza kwenye Epiq Open Mic jijini Dar

Mamia ya vijana jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita walijitokeza kushiriki kuonesha vipaji vyao vya uimbaji kwenye shindano la Epiq Open Mic linaloandaliwa na Marco Chali Foundation na lililofanyika makao makuu ya Zantel. Hizi ni baadhi ya picha.

Godzilla akimuonyesha mmoja wa washiriki namna ya kuchana
Godzilla akimuonyesha mmoja wa washiriki namna ya kuchana

Huku ikiwa imebaki wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu mya wa Epiq BSS, Zantel kwa kushirikana na Marco Chali Foundation, wamezindua Epiq Open Mic ili kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.

Fursa hii, ya Epiq Open Mic, inawapa nafasi vijana wenye vipaji vya muziki fursa ya kusikilizwa na mtayarishaji wa muziki maarufu nchini, Marco Chali pamoja na jopo la wanamuziki kama Godzila na Dknob, ambao wanawashauri mambo kadhaa kuhusiana na muziki wao, na huku wale wenye vipaji zaidi wakipewa nafasi ya kurekodi na Marco Chali.

Jopo la washauri likiwa linamsikiliza mmoja wa washiriki. Kutoka kulia ni Godzilla, Marco Chali, Dknob na Walter.
Jopo la washauri likiwa linamsikiliza mmoja wa washiriki. Kutoka kulia ni Godzilla, Marco Chali, Dknob na Walter

Jopo la washauri likongozwa na Marco Chali (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Dknob, Walter na mwisho kulia ni Godzila
Jopo la washauri likongozwa na Marco Chali (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Dknob, Walter na mwisho kulia ni Godzila

Mdada akionyesha uwezo wake mbele ya washauri
Mdada akionyesha uwezo wake mbele ya washauri

Akizungumzia Epiq Open Mic, Marco Chali anasema hii ni fursa ya vijana kujifunza misingi ya muziki, lakini pia kuweza kurekodiwa muziki wao.

‘Lengo la Epiq Open Mic ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisema Chali..

Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.

Mmoja wa vijana akiimba mbele ya washauri
Mmoja wa vijana akiimba mbele ya washauri

Mmoja wa wasichana akionyesha uwezo wake
Mmoja wa wasichana akionyesha uwezo wake

Kwa upande wake, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.

‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.

Vijana waliojitokeza wakijiandikisha
Vijana waliojitokeza wakijiandikisha

Vijana waliojitokeza wakiwa kwenye foleni.
Vijana waliojitokeza wakiwa kwenye foleni

Wasichana walijitokeza kwa wingi
Wasichana walijitokeza kwa wingi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents