Promotion

Picha: Maonyesho ya uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyodhaminiwa na NMB yafana

photo1
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa (kushoto) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga 26-27/9/2013. Walioambatana naye ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Nagu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Mh. Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Mkutano wa Uwekezaji Nd. Salum Shamte pamoja na viongozi na washiriki wengine

photo2
Naibu Waziri TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho hayo. Kutoka kulia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo, Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa pamoja na wafanyakazi wa NMB Tawi la Madaraka Tanga

photo3
Mkurugenzi Ukaguzi wa ndani wa Makampuni ya Impala Bw. Julius Makara (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Wateja Wakubwa Bw. Nsolo Mlozi baada ya kutembelea banda la NMB

photo4
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pangani Farms Bw. Charles Makoi
photo5
Mkurugenzi Mtendaji wa Pride (T) Limited Bw. James Obama (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo. Pembeni yake ni Meneja wa Tawi la NMB Madaraka Tanga Bw. Juma Mpimbi, Meneja Uwekezaji wa NSSF Bw. Abdallah Mseli na Meneja Mahusiano Wateja Wakubwa Bi. Shilla Senkoro katika maonesho hayo
photo6
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Majid Mwanga (kati) akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga

Photo7
Mbunge wa Kilindi Mh. Beatrice Shelukindo akiwa na maofisa wa NMB alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents