Burudani

Picha: Mastaa wanne wa muziki waliojiunga na siasa Kenya

Wakati uchaguzi mkuu nchini Kenya ukiwa umebakiza miezi minne pekee, joto la kisiasa nchini Kenya limezidi huku kila upande wa vyama vya kisiasa ukipiga kifua kuchukua hatamu za uongozi.

Kulingana na katiba ya nchini Kenya, uaniaji wa nafasi za ungozi uliongezeka kwani sasa kuna nafasi za Useneta na Ugavana kinyume na ilivyokuwa kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2002, ambapo wakenya waliwachagua madiwani (MCA Member of county Assembly kwa sasa), Mbunge, na Rais. Kwa sasa wakenya kulingana na katiba wanatakiwa kuchagua MCA, Wawakilishi wakinamama, mbunge, Seneta, Gavana na Rais akiwa na makamu wake. Kutokana na hivi, nimekusogezea wasanii wakali kutoka Kenya wenye kumezea nafasi tofauti za kisiasa kwenye uchaguzi ujao wa Agosti 8 2017.

1. Jaguar

Kwa sasa anatamba na ngoma African Warrior aliyomshirikisha msanii EL kutoka nchini Ghana. Jaguar ameamua kupigania kiti cha eneo bunge la starehe Jijini Nairobi ambacho kwa sasa kinakaliwa na mwanasiasa nguli Maina Kamanda. Tayari Jaguar majuma kadhaa yaliyopita, alijiuzulu kama mmoja wa ma directors wa NACADA ili kuanza rasmi kazi ya kupiga kampeni ya kuwania kiti hicho.

2. Prince Adio

Ni mmoja ya legendary katika muziki wa kizazi kipya ni nikimweka kundi moja na Nyota Ndogo, waliowahi kufungulia njia mastaa wanaoibuka nchini Kenya. Alitamba na vibao kama Nikiwa Ndani, Natamani, Sikitiko na vingine vingi. Pia ni muigizaji ambaye amewahi kuonekana kwenye tamthilia zinazorushwa hewani na televisheni nchini Kenya kama vile tamthilia ya Udhalimu na nyinginezo. Kwa sasa anawania kiti cha MCA wadi ya Frere Town Mombasa mjini.

3. Cannibal

Ni rapper mkali kutoka Mombasa ambaye wengi watakuwa wanamkubali kwa jinsi anavyofoka. Cannibal aliwika na ngoma aliyomshirikisha rapper mwenzake Sharam enzi hizo na kutoa hit kama Street Hustler, Bouncing, Kichwa Kibovu na nyinginezo. Kwa sasa pia anajiunga na mastaa kama Jaguar katika mtanange wa kisiasa na kupigania kiti cha MCA wadi ya Mtopanga Mombasa mjini.

4. Frasha

Kutoka kundi maarufu la muziki la P-UNIT, Frasha ambaye ni staa wa muziki kutoka hapa nchini Kenya, pia hajaachwa nyuma. Ameweka wazi kuwa atapigania kiti cha MCA wadi ya Athi River Township, huku tayari akiwa ametangaza rasmi chama cha kisiasa atakachokitumia katika mtanage huo na chama chenyewe ni chama cha Maendeleo Chap Chap kinachoongozwa na Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutia.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents