Picha

Picha: Mazishi ya Chris yalivyohudhuriwa na mastaa mbalimbali

By  | 

Hatimaye safari ya kuupumzisha mwili wa mwanamuziki na muandishi wa mashairi Chris Cornell’s imefikia tamati hapo jana katika maeneo ya Hollywood Forever Cemetery.

Katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na watu wa karibu na familia ya marehemu pamoja na watu maarufu kama vile Brad Pitt, Pharrell, Dave Grohl, Lisa Marie Presley, Dave Navarro, Jimmy Page, Courtney Love, Gavin Rossdale, James Franco, Christian Bale, Josh Brolin, Billy Idol, Joe Walsh, Lars Ulrich, James Hetfield, na waimbaji wenzake Tom Morello, Pearl Jam’s Jeff Ament and Matt Cameron, Linkin Park’s Chester Bennington and Brad Delson, Soundgarden’s Kim Thayil and Brolin.

 

 

Pia mke wa marehemu, Vick naye alikuwepo kwenye mazishi hayo licha ya kuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kifo cha mumewe ambacho kilitokea  May 18 katika maeneo ya MGM Grand Hotel ambako marehemu alikutwa amefariki bafuni.

Pia Vick alieleza kuwa aliongea na mume wake kwa njia ya simu kabla ya umauti kumkuta alipomaliza tamasha lake la Detriot. Kwa mujibu wa familia ya Chris imeeleza kuwa marehemu aliwahi kukiri kuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya.

Chris ambaye ametamba na nyimbo kadhaa ikiwemo ya Nearly Forgot My Broken Heart aliyotoka mwaka 2015, amezikwa karibu na kaburi la marehemu Johnny Ramone, ambaye naye alikuwa mwanamuziki na mpiga gitaa aliyefariki mwaka 2004, septemba15.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments