Burudani

Picha: Miriam Ntakisivya atoa msaada kwa Kigoma Sisterz

Miriam Ntakisivya ambaye ni Mwanamitindo, video vixen na pia ni Mwakilishi UWT vijana katika Mkoa wa Kigoma, amekabidhi msaada kwa timu ya soka ya wanawake ya Kigoma Sisterz.


Miriam Ntakisivya akimkabidhi msaada kwa kepteni Sophia Mwasikili

Katika kukabidhi msaada huo ambao ulipokelewa na kepteni wa timu hiyo Sophia Mwasikili, Miriam aliambatana na kaimu Katibu wa vijana wa mkoa huo Adam Kagoma.

Zawadi ambazo wametoa kwa timu hiyo ni chakula, mafuta na katoni za maji ya kunywa. Viongozi hao wamefanya hilo ni kutokana na kusikiliza kilio cha timu hiyo ambacho kinawachezaji zaidi ya wanne wanaocheza timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars).

Hata hivyo viongozi hao wamewaomba watu waendelee kujitolea kuisaidia timu hiyo ambayo inayofanya vizuri. Wakati huo huo mrembo Mirim amepotoa pongezi za dhati kwa Miss Ubungo 2014, Diana Kato kwa kuchangia alichoguswa katika msaada huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents