Michezo

Picha: Mourinho afanya sherehe ya kipekee baada ya kuongezewa mkataba Man United

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho hapo jana siku ya Alhamisi ameonekana akisherehekea kwa staili ya kipekee baada ya kuongezewa kandarasi ya kusalia ndani ya timu hiyo.

 

Mourinho amesaini kandarasi itakayomfanya kuendelea kusalia Old Trafford mpaka mwaka 2020 baada ya ule wa awali kutarajiwa kumalizika 2019 kufuatia kitendo hicho meneja huyo raia wa Ureno aliamua kwenda kupata chakula kama seheme ya sherehe yake katika mgahawa wa Kihispania uliyopo katikati ya mji unaomilikiwa na kiungo wa Man United, Juan Mata na baba yake Juan Manuel.

Picha kadhaa zimemuonesha Mourinho akiondoka katika mgahawa huo usiku wa Alhamisi kabla ya kurejea Lowry Hotel sehemu ambayo ndipo alipopangiwa akiwa ndani Manchester.

Jose Mourinho amesafiri na kikosi chake alfajiri ya leo kwenda kuikabili Yeovil katika michuano ya FA Cup mchezo wa mzunguko wan ne utakaopigwa katika dimba la  Huish Park.

Boss huyo wa United amethibitisha kuwa mshambuliaji wao mpya Alexis Sanchez atakuwa sehemu ya wachezaji watakao kuwepo katika mchezo huo.

Huku akisema kuwa kuwasili kwa Sanchez kutawafanya wachezaji wake Mata, Romelu Lukaku, Anthony Martial na Marcus Rashford kujituma zaidi uwanjani ilikujihakikishia kupata namba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents