Picha

Picha mpya ya mtoto wa Beyonce, Blue Ivy yaleak mtandaoni


Kwa muda mrefu picha inayomwonesha mtoto wa Beyonce na Jay-Z usoni haijaonekana tangu watoe picha za awali kabisa alipozaliwa mtoto huyo.

Mara nyingi picha ambazo zimekuwa zikionekana ni zile ambazo zinamwonesha akiwa amefunikwa na wazazi wake.

Na sasa kuna picha ambayo imesambaa kwenye mtandao inayomwonesha mtoto huyo sura yake ilivyo sasa na anaonekana amekua sana.

Picha hiyo inamwonesha Beyonce akiwa amembeba mwanae huyo mwenye miezi sita sasa wakati akiongea na wafanyakazi katika duka la Bergdorf Goodman jijini New York.

Akiwa ndani Bey aliifunua baby show ambayo humfunika nayo mara kwa mara na kumpa nafasi mpiga picha aliyekuwa amejificha kupata picha ya kwanza inayoonesha sura ya Blue tangu zile zilizotolewa mwenzi February.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents