Burudani

Picha: Msanii Bobi Wine ala kiapo cha ubunge leo

By  | 

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda na mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki , Robert Kyagulanyi Ssentamu ameapishwa leo katika bunge la nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa New Vison wa nchini humo umesema, Bobi wakati wa kuapishwa amesema anaingia katika bunge hilo kama kiongozi na sio mwanasiasa kama ilivyokuwa kwa viongozi wengine bungeni.

Wine amesindikizwa bungeni asubuhi ya leo na mamia ya mashabiki wake walioongozwa na mkewe Barbara Itungo (Barbie), kaka zake Eddy Yawe na Nyanzi, msanii Hilderman na watu wengine wa karibu.

Muimbaji huyo alishinda kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika takribani wiki mbili zilizopita katika jimbo hilo na kufanikiwa kuwabwaga wagombea wengine wanne kwa kupata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa na wananchi wa eneo hilo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments