BurudaniUncategorized

Picha: Mtanzania Emanuel Austin aiongeza shule yake ya dance Ujerumani

Tanzania imejaaliwa vipaji vingi vinavyoitangaza nchi katika majukwaa ya mbalimbali ya kimataifa. Mmoja wa mabalozi muhimu wa Bongo ni Emanuel Austin ambaye yeye pamoja na mke wake, Larissa Bertsch wana chuo kikubwa cha dance mjini Frankfurt, Ujerumani.

Lakini kubwa zaidi kwa wawili hao wamefanikiwa kupiga hatua nyingine katika chuo chao baada ya wikiendi hii kufanya sherehe ya ufunguzi wa chuo chao ambacho kwa sasa wametafuta eneo kubwa zaidi tofauti na kilivyokuwa mwanzoni ambapo kina uwezo wa kuchukuwa watu wengi zaidi pamoja na ukumbi wa kufanyia matamasha makubwa.

Akiongea na Bongo5, Austin amesema, “Zamani ilikuwa ni chuo tu, sasa hivi nimefanya chuo na events ambapo tumefanya na designer ambao wamefanya chuo kiwe kama event hall. Kwa hiyo sasa hivi nafanya chuo na usiku inakuja dance party na something special party kama hivyo.”


Emanuel Austin (wakwanza kulia) na mkewe Larissa (mwenye gauni nyekundu) wakiwa na wageni waliohuduria katika sherehe ya ufunguzi wa chuo chao kikubwa

“Zamani kwenye chuo changu sio watu wengi walikuwa wanweza kupaki nje, sikuwa na park station ya gari. Lakini sasa hivi watu wanaweza kupark direct pale kwenye chuo, hiyo ilikuwa ni wazo jingine ambalo lilinifanya intake kubadili. Nilianza na location ndogo sana lakini sasa hivi imekuwa kubwa sana watu wengi wanakuja kucheza kwenya dance school yangu ndio maana tulichagua eneo kubwa mimi na mke wangi Larissa,” ameongeza.

Tazama picha zaidi za chuo hiko:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents