Picha: Mtanzania Emanuel Austin na shule yake ya dance afanya hafla iliyohudhuriwa na watu 15,000 Ujerumani

Tanzania imejaaliwa vipaji vingi vinavyoitangaza nchi katika majukwaa ya kimataifa.

Hafla kama hii inayoandaliwa na Austin na mke wake hufanyika takriban mara mbili kwa mwaka na hufana sana.

Mmoja wa mabalozi muhimu wa Bongo ni Emanuel Austin ambaye yeye pamoja na mke wake, Larissa Bertsch wana chuo kikubwa cha dance mjini Frankfurt, Ujerumani.

 

Jumamosi, March 18, walianda hafla kubwa mjini humo iliyohusisha maenesho ya kucheza ya wanafunzi wa shule yake na kuhudhuriwa na takriban watu 15,000. Shule yake ni kubwa zaidi katika masuala ya dance nchini Ujerumani.

“Nawashukuru sana watu wote waliokuja kwenye event hiyo kuja kuona shows. Kiukweli ilifanikiwa sana,” ameiambia Bongo5. “Pia namshukuru Mungu, familia pamoja na marafiki zangu kwa kuniunga mkono.”

Tazama picha zaidi za hafla hiyo:


Pichani ni Emanuel Austin (wa pili kulia) na mke wake Larissa (wa kwanza kushoto) wakiwa na watu wao karibu


Emanuel Austin akiwa na mke wake Larissa


Baadhi ya wanafunzi wa Tanzschuleweiss wakionesha uwezo wao


Emanuel Austin akizungumza kwenye hafla hiyo

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW