Burudani

Picha: Mzungu Kichaa akionyesha hisia zake kwenye muziki

Msanii wa muziki mwenye asili ya Denmark, Mzungu Kichaa leo ameendeleza kutoa burudani ya muziki wa ‘live’ katika tamasha kubwa la muziki Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla la Sauti za Busara linalofanyika kisiwani Zanzibar.

Msani huyohakusita kuonuesha hisia zake tofauti tofauti za kuufurahia muziki huo ambao umekuwa ukimpa umaarufu zaidi kutokana na uimbaji wake kwa lugha ya kiswahili.

Awali kabla ya Mzungu Kichaa kutoa burudani vikundi vingine vya ngoma za asili kutoka sehemu tofauti duniani vilipata nafasi ya kuonyesha utamaduni wao na uchezaji wa muziki katika maeneo tofauti yaliyopangwa kama vile:- Bustani ya Forodhani na Ngome Kongwe.

Tamasha la Sauti za Busara lilifunguliwa rasmi hapo jana (08,02,2017) na litadumu kwa siku nne mfululizo huku wasanii zaidi ya 400 wakitarajiwa kutoa burudani ya muziki live.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents