Burudani

Picha: Nay awasha moto kwenye show ya ‘Wapo Tour’ Dar Live

Msanii wa muziki wa hip hop,Nay wa Mitego amewakata kiu mashabiki wa muziki wake wa jiji la Dar es salaam kupitia show yake ya ‘Wapo Tour’ iliyofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam.

Nay wa Mitego

Rapa huyo alisindikizwa na wasanii kama Shilole, Kala Jeremiah,Wakali Wao, Edu Boy, Forb pamoja na wasanii wengine wachanga.

Kabla ya show hiyo kuanza mvua kubwa ilinyesha na kusababisha baadhi ya mashabiki kusita kuingia lakini baada ya nusu saa mvua hiyo ilikatika na mashabiki kuigia kwa wingi.
Mashabiki wakicheza bila kujali mvua

Akiongea na Bongo5 muda mchache baada ya kumalizika kwa show hiyo, Nay aliwashukuru mashabiki wake kwa kujitokeza kwa wingi licha ya mvua kubwa kunyesha mapema kabla ya show kuanza.

“Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kujitokeza kwa wingi na kunionyesha upendo wao wa dhati. Mvua imenyesha kubwa lakini mashabiki walibaki kwaajili ya kuangalia show yangu hicho ni kitu kikubwa sana,” alisema Nay.

Barnaba

Wakali Wao wakifanya yao

Barnaba na Shilole
Barnaba na Shishi Baby
Nay na mashabiki wake


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents