Habari

Picha: Nyalandu apokea matembezi ya kupinga ujangili kutoka Arusha hadi Dar

Safari kati ya Arusha na Dar es Salaam yenye umbali wa zaidi ya kilomita 650 kwa basi inaweza kuchukua zaidi ya masaa 8, umewahi kujiuliza kwa kutembea kwa miguu unaweza kuchukua muda gani?

s (11)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu (anayeongea na simu) akiongoza matembezi ya kupinga ujangili kuelekea mnazi mmoja baada ya kuyapkea Ubungo, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na wadau wengine katika mapambano ya ujangili

Lakini uthubutu na nia njema yenye uzalendo ndani yake ndivyo vilivyowafanya watu 18 washiriki katika matembezi ya kupinga ujangili nchini “Walk for Elephants.

s (1)

Matembezi hayo ambayo yamepewa jina la “Walk for Elephants” yamedumu kwa muda wa siku 19 kabla ya kupokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Alhamisi ya Septemba 12.

s (2)

Nyalandu ameunga mkono uzalendo huo kwa vitendo pale alipotembea kwa mguu kutoka Ubungo hadi Mnazi Mmoja na kutumia zaidi ya saa moja na nusu akiambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mkurugenzi wa idara ya wanyama pori, Profesa Alexender Songorwa pamoja na Mkurugenzi wa African Wildlife Trust, Pratik Patel.

s (10)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati), akiwa na wadau wa vita dhidi ya ujangili, Kulia kwake ni Meneja wa maendeleo ya jamii kutoka Friedrikin Group of Comanies, Aurelia Mtui, upande wa kushoto wa Nyalandu ni Faraja Nyalandu na Nancy Sumari pamoja na askari wanyama pori kutoka Arusha

Nyalandu alisema matembezi hayo ya kupiga vita ujangili nchini yamefanyika wakati ambapo kuna ongezeko kubwa la ujangili, nchini hususan ujangili wa tembo.

Ujangili huo husababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya meno ya tembo katika masoko haramu huko Mashariki ya Kati na Asia na Kuimarika na kuongezeka kwa magenge ya ujangili (poaching syndicates) pamoja na ubora wa mawasiliano.

Sababu nyingine ni kudorora kwa uchumi na kuongezeka kwa umaskini katika jamii na kufanya watu wengi kujiingiza kwenye ujangili cha uhalifu mwingine, uroho wa kutaka utajiri wa haraka ambao umewafanya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo na watumishi wa umma kujiingiza katika ujangili na rushwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa jumla.

s (7)
Naibu Waziri, Lazaro Nyalandu akipokea hundi ya dola za kimarekani milioni 250 kutoka kwa Mkurugenzi wa Conservation Fund, Mitchel Allard kwaajili ya kutekeleza shuguhuli za vita dhidi ya ujangili

Ujangili umechangia katika kupungua idadi ya tembo nchini kutoka 350,000 miaka ya 1960 hadi 110,000 mwaka 2009. Idadi ya tembo wanaouawa na majangili inazidi kuongezeka kila mwaka.

Matembezi hayo yaliyoandaliwa na shirika la African Wildlife Trust yamehitimishwa leo ambapo wadau mbalimbali na wananchi walifika kuwaona mashujaa waliotembea katika safari hiyo.

Story: Dotto Kahindi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents